London, England
Kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp (pichani) amempongeza kocha wa sasa wa timu hiyo, Arne Slot baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu England (EPL) msimu huu wa 2024-25.
Liverpool ililibeba taji la EPL juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Anfield baada ya kuilaza Tottenham Hotspur 5-1 mabao 5-1, huu ukiwa ni msimu wa kwanza wa Slot na timu hiyo.
Kocha huyo amefanikiwa kubeba taji hilo huku akiweka rekodi ya kufanya hivyo wakati timu yake bado ina mechi nne kabla ya kumalizika kwa mechi zote za msimu.
Slot alikabidhiwa jukumu la kuinoa Liverpool mwaka jana majira ya kiangazi na amebeba taji hilo kwa rekodi nzuri ya kupoteza mechi mbili tu na hilo ni jambo mojawapo lililomvutia Klopp hadi kumpa pongezi.
“Hongera umefanya vizuri sana sana, ni furaha ya mambo ya sasa na utayari kwa mambo yajayo, hongera,” alisema Klopp kupitia mtandao wa Instagram.
Wakati wakishangilia ushindi huo kwenye dimba la Anfield, Slot akiwa mwingi wa tabasamu aliimba wimbo uliotaja jina la Klopp na kutoa salamu zake za shukrani kwa mtangulizi wake huyo kabla ya kufurahia na mashabiki.
Klopp amekuwa kocha wa Liverpool kwa kipindi cha miaka tisa kati ya mwaka 2015 hadi 2024 alipoachia ngazi na kukabidhia jukumu hilo Slot na kwa kipindi chake ametwaa mataji ya FA, Ligi ya Mabingwa Ulaya na EPL.
Kimataifa Klopp ampongeza Slot
Klopp ampongeza Slot
Read also