Na mwandishi wetu
Yanga wameanza vyema mbio za kulisaka Kombe la Muungano baada ya kuilaza KVZ mabao 2-0 mechi iliyochezwa Jumamosi hii, Aprili 26, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Kwa ushindi huo Yanga ambao pia ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC wanakuwa wamefuzu moja kwa moja hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea visiwani Zanzibar.
Yanga walianza kulichachafya mapema lango na KVZ kabla ya kuandika bao la kwanza katika dakika ya 27 lililofungwa na Stephane Aziz Ki kwa pasi ya Dennis Nkane.
Baada ya kutoa pasi iliyozaa bao, nyota ya Nkane iling’ara kwa mara nyingine katika dakika ya 86 alipoifungia Yanga bao la pili na la ushindi.
Katika mechi ya nusu fainali Yanga itacheza Jumanne ijayo na JKU ambayo ilifanikiwa kuitoa Singida Black Stars katika mechi nyingine ya robo fainali.
Mechi nyingine ya nusu fainali itapigwa Jumatatu kati ya Azam FC na Zimamoto ambayo ilifuzu hatua hiyo kwa kuitoa Coastal Union kwa bao 1-0 wakati Azam nayo iliitoa KMKM pia kwa bao 1-0.
Kimataifa Yanga yaitoa KVZ Kombe la Muungano
Yanga yaitoa KVZ Kombe la Muungano
Read also