Na mwandishi wetu
Yanga imeipa kipigo cha mabao 4-0 Fountain Gate FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Jumatatu Aprili 21, 2025 kwenye Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa mjini Manyara.
Yanga ilianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 38 lililofungwa na Clement Mzize ambaye aliyatumia vizuri makosa ya kipa wa Fountain Gate, John Noble kuipatia Yanga bao.
Bao la pili la Yanga lilifungwa na Stephane Aziz Ki ambaye kama ilivyo kwa Mzize naye aliyatumia makosa ya kipa Noble aliyejichanganya wakati akiokoa mpira ulioelekezwa langoni mwake badala yake akamrudishia mfungaji.
Kipindi cha pili kiliendelea kuwa kigumu kwa Fountain Gate baada ya kupachikwa bao la tatu mfungaji akiwa Mzize katika dakika ya 69 akiitumia pasi ya Jonathan Ikangalombo.
Mzize ambaye pia aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo, bao hilo lina maana kubwa kwake kwani sasa amefikisha mabao 13 katika ligi hivyo kuwa kinara akifuatiwa na Jean Ahoua wa Simba mwenye mabao 12 sawa na Prince Dube wa Yanga.
Clatous Chama alikamilisha bao la nne kwa Yanga katika dakika ya 89 akifunga kwa mpira wa adhabu iliyotolewa baada ya Mtenje Albano kumchezea rafu Mzize nje kidogo ya eneo la penalti.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 70 katika mechi 26 ikiiacha Simba nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 katika mechi 22.
Kimataifa Yanga yaicharaza Fountain Gate mabao 4-0
Yanga yaicharaza Fountain Gate mabao 4-0
Read also