Na mwandishi wetu
Mwamuzi wa kimataifa, Ahmed Arajiga ndiye atakayewahukumu mahasimu wa soka nchini Tanzania Yanga na Simba watakapokutana Machi 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, katika mechi hiyo Arajiga ambaye anatokea mkoani Manyara atasaidiwa na Mohamed Mkono wa Tanga na Kassim Mpanga wa Dar es Salaam wakati kamishna wa mchezo ni Salim Singano wa Tanga.
Arajiga ni mmoja wa waamuzi waliojijengea heshima nchini na mashabiki wengi wanaamini ana sifa za kupewa mechi hiyo ambayo huandamana na vitimbwi vya ndani na nje ya uwanja kuanzia kwa mashabiki hadi wachezaji.
Mechi hiyo itakuwa ni ya mwisho katika Ligi Kuu NBC msimu huu wa 2024-25 kwa timu hizo ambapo katika mechi ya kwanza Simba ililala kwa bao 1-0.
Simba na Yanga zinaumana zikiwa katika nafasi za juu kwenye ligi hiyo, Yanga ikishika usukani na pointi 58 na Simba inashika nafasi ya pili na pointi 54 ingawa Yanga imecheza mechi 22 wakati Simba imecheza mechi 21.
Kwa msimamo wa ligi ulivyo, matokeo ya mechi hiyo yanatafsiriwa na mashabiki walio wengi kwamba yanaweza kutoa mwelekeo wa nanio anaelekea kubeba taji la ligi hiyo kwa msimu huu.
Soka Arajiga kuzihukumu Simba, Yanga
Arajiga kuzihukumu Simba, Yanga
Related posts
Read also