Na mwandishi wetu
Waamuzi wa soka 20 wanatarajia kushiriki kozi maalum ya teknolojia ya VAR ambayo itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 3 hadi 7 mwaka huu.
Taarifa iliyopatikana kwenye vyanzo mbalimbali vya habari vya TFF imewataja waamuzi hao kuwa ni Ahmed Arajiga, Henry Sasii, Tatu Malogo, Nassir Siyah, Ramadhan Kayoko na Mohammed Simba.
Waamuzi wengine ni Hamdan Said, Ally Ramadhan, Kassin Seif, Frank Komba, Alex Pangras, Abdallah Mwinyimkuu, Ester Adabert na Amina Kyando.
Wengine waliomo kwenye orodha hiyo ni Shaaban Mussa, Janeth Balama, Mohammed Mkono, Glory Tesha, Zawadi Yusuph na Siraji Mkwaju.
Kozi hiyo huenda ikawa mwanzo wa teknolojia ya VAR kuanza kutumika katika mechi za soka nchini hasa baada ya TFF kuahidi takriban miaka miwili iliyopita kwamba ina mpango wa kuanza kuitumia teknolojia hiyo.
Hoja ya utumiaji wa VAR imewahi pia kujadiliwa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali kulazimika kutoa ufafanuzi wa lini hasa teknolojia hiyo ingeanza baada ya muda mrefu kupitia tangu ahadi hiyo itolewe.
Teknolojia ya VAR inamsaidia mwamuzi kufikia maamuzi sahihi kwa kutumia picha za video zilizorekodiwa kwa kusimamisha mchezo na kujiridhisha kupitia picha hizo baada ya kuhisi kuna utata katika baadhi ya matukio ya uwanjani.
Kimataifa Waamuzi 20 kushiriki kozi ya VAR
Waamuzi 20 kushiriki kozi ya VAR
Read also
