Na mwandishi wetu
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC, Yanga wameendelea na kasi yao ya kulisaka taji la ligi hiyo baada ya kuinyuka Pamba Jiji mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa Ijumaa hii kwenye dimba la CCM Kirumba mjini Mwanza.
Ushindi huo umeifanya Yanga kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa wamefikisha pointi 58 na kuendelea kuimarisha matumaini yao ya kulitetea taji.
Yanga inafuatiwa na Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 51 ingawa Yanga imecheza michezo 22 ikiwa imewazidi Simba kwa michezo miwili.
Beki wa kushoto Shedrack Boka ndiye aliyekuwa wa kwanza kuziona nyavu za Pamba baada ya kuandika bao la kwanza katika dakika ya 27 kwa mpira wa adhabu.
Baada ya hapo mabao mengine ya Yanga yalifungwa na Stephane Aziz Ki ambaye aliingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Khalid Aucho.
Aziz Ki aliifungia Yanga bao la pili kwa kichwa dakika ya 74 kabla ya kuongeza bao la tatu dakika tatu baadaye kwa shuti kali la nje ya 18.
Soka Yanga yaitandika Pamba 3-0
Yanga yaitandika Pamba 3-0
Read also