Na mwandishi wetu
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Walace Karia ametuma salamu za pole kwa timu ya Dodoma Jiji baada ya kikosi cha timu hiyo kupata ajali ya gari, leo Jumatatu, Februari 10, 2025.
Msafara wa timu hiyo ulipata ajali majira ya saa nne asubuhi eneo la Nangulukuru mkoani Lindi wakati wakitokea Ruangwa kwenye mechi yao ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Namungo kwenye Uwanja wa Majaliwa.
Katika salamu hizo zilizotolewa kupitia taarifa ya TFF iliyosainiwa na ofisa habari wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo, Karia amewatakia heri majeruhi wote wapone na kurejea katika majukumu yao kama kawaida.
Katika ajali hiyo hakuna taarifa yoyote ya kifo iliyotangazwa zaidi ya majeruhi ambao nao inadaiwa hawako katika hali mbaya sana.
Soka Karia awapa pole, Dom Jiji
Karia awapa pole, Dom Jiji
Read also