Na mwandishi wetu
Kipigo cha mabao 2-0 ilichokipata Kilimanjaro Stars mbele ya timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars kimetosha kuitoa timu hjyo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Kili Stars imepokea kipigo hicho Jumanne hii usiku kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba na hivyo kuwa kipigo cha pili baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi dhidi ya wenyeji Zanzibar Heroes.
Mashujaa wa Harambee Stars katika mchezo dhidi ya Kili Stars walikuwa ni Boniface Muchiri aliyefunga bao la kwanza dakika ya 56 na Ryam Ogam aliyefunga bao la pili dakika ya 67.
Harambee sasa inasubiri kuumana na wenyeji Zanzibar mechi ambayo itapigwa Ijumaa hii usiku kwenye Uwanja wa Gombani.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi msimu huu imezishirikisha timu za taifa badala ya klabu kama ilivyozoeleka kwa misimu iliyopita.
Kimataifa Harambee yaitambia Kili Stars Mapinduzi Cup
Harambee yaitambia Kili Stars Mapinduzi Cup
Read also
