Madrid, Hispania
Nyota wa Real Madrid, Vinícius Júnior ameomba radhi baada ya kupewa kadi nyekundu jana Ijumaa wakati timu yake ikiumana na Valencia katika La Liga na kupata ushindi wa 2-1.
Katika mechi hiyo Valencia wakiwa nyumbani walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Hugo Duro kabla ya Madrid kujikuta katika majanga kwa Jude Bellingham kukosa penalti baada ya mkwaju aliopiga kugonga mwamba.
Baada ya hapo mshambuliaji wao mpya, Kylian Mbappe alifunga bao ambalo baadaye mwamuzi alilikataa kwa madai kuwa mfungaji aliotea.
Wakati Madrid ikipambana ilipata pigo baada ya Vinícius kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea ndivyo sivyo kipa wa Valencia, Stole Dimitrievski.
Madrid hata hivyo baadaye ilinusuriwa kwa bao la kusawazisha dakika ya 85 mfungaji akiwa Luka Modric aliyeingia akitokea benchi wakati bao la ushindi la timu hiyo lilifungwa na Bellingham katika dakika za nyongeza.
“Samahani na asanteni wenzangu,” alisema Vinícius Jr baada ya mechi hiyo kupitia taarifa yake iliyowekwa kwenye mtandao wa X zamani Twitter.
Vinicius Jr hata hivyo alionesha hasira mara baada ya kupewa kadi hiyo dakika ya 79 na alizuiwa na wachezaji wenzake Antonio Rudiger na kocha wa makipa, Luis Liopsis wakati akitaka kumfuata mwamuzi.
Naye kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alisema kwamba kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwao lakini aliwapongeza wachezaji wake kwa jinsi walivyoweza kujibu mapigo baada ya kukosa penalti na goli lao kukataliwa.
Kimataifa Vinicius aomba radhi kwa kupewa red card
Vinicius aomba radhi kwa kupewa red card
Read also
