Cardiff, Wales
Hali bado tete kwa kiungo wa timu ya taifa ya Wales, Aaron Ramsey ambaye anapambana na muda ili kuwa fiti na kuiwakilisha timu hiyo kwenye mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.
Ramsey, 34, ambaye pia anaichezea Cardiff City hajacheza mechi yoyote ya ushindani tangu Septemba mwaka jana alipoumia misuli wakati akiiwakilisha Wales kwenye mechi dhidi ya Montenegro.
Awali ilielezwa kwamba Ramsey angekuwa fiti baada ya miezi miwili na ingawa alianza mazoezi na timu ya Cardiff lakini siku chache baadaye mambo yaligeuka na kuwa hovyo.
Kwa sasa nyota huyo wa zamani wa timu za Arsenal na Juventus anapambana na muda ili kuiwakilisha Wales kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Kazakhstan ambayo itapigwa Machi 22.
“Aaron bado anapambana kwenye matibabu, kupona kwake kwa kiasi fulani kumekuwa kwa taratibu kwa sababu amepata majeraha na hana presha, nadhani hadi Machi atakuwa sawa,” alisema kocha wa Cardiff, Omer Riza.
Riza pia alisema kwamba timu yake itamkosa kiungo wake mwingine, David Turnbull ambaye naye alifanyiwa upasuaji wa misuli baada ya kuumia Desemba mwaka 2024 na huenda akakosa mechi zote zilizobaki za msimu huu.
Kimataifa Majeruhi Ramsey hali tete
Majeruhi Ramsey hali tete
Related posts
Read also
