Manchester, England
Kocha wa Man City, Pep Guardiola amesema wanatakiwa kuacha kufikiri kubeba taji la tano mfululizo wakati huu timu hiyo ikiandamwa na mikosi ya matokeo mabaya.
Man City Jumamosi imetoka sare ya mabao 2-2 na Crystal Palace katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) ambapo ilijikuta ikipambana hadi kusawazisha mabao hayo moja baada ya jingine.
Pep hata hivyo alijivunia timu yake kwa kupata pointi baada ya kupambana kwa namna ya kipekee hadi kusawazisha mara mbili na kukiri kwamba huu ni msimu mgumu ingawa alisema ni vyema kusubiri miezi ya mwisho.
“Kwa sasa hatuwezi kuzungumzia mbio za kulisaka taji kwani tumepoteza mechi nne mfululizo, tutajitahidi wachezaji wakae sawa, yote yatajulikana mwezi wa mwisho,” alisema Pep.
Mabao yaliyoiokoa Man City katika mechi hiyo yalifungwa na Rico Lewis na Erling Haaland na kuipa timu hiyo sare ambayo Pep amewasifia wachezaji wake akijivunia utulivu wao wakati huu timu hiyo ikiandamwa na janga la wachezaji majeruhi.
“Tuna wachezaji wengi muhimu majeruhi na wale wenye mechi nyingi lakini utimamu wao kimwili unauona na tulifanya kila tulichoweza ili kushinda na kwa hilo najivunia wachezaji wangu,” alisema Pep.
Kwa sasa Man City wanajiandaa kwa mechi ngumu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus ambayo itapigwa Desemba 11, 2024.
Kimataifa Pep apotezea mbio za ubingwa
Pep apotezea mbio za ubingwa
Read also
