Na mwandishi wetu
Kocha wa Azam FC, Rachid Taoussi ameibuka kinara wa tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu NBC kwa mwezi Novemba akiwabwaga Fadlu Davids wa Simba na Hamad Ali wa JKT Tanzania.
Taoussi ameiongoza vyema timu yake kushinda michezo yote mitatu ya kipindi hicho na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya nne hadi ya pili na hatimaye kushika usukani.
Katika mechi hizo Azam iliumana na Singida Black Stars na kuichapa mabao 2-1 kabla ya kuzifunga Yanga bao 1- 0 na Kagera Sugar bao 1-0.
Naye mshambuliaji wa Tabora United, Offen Chikola amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba baada ya kuonesha kiwango kizuri akiwashinda kipa Mussa Camara wa Simba na mchezaji mwenzake wa Tabora United, Yacouba Sogne.
Katika kipindi hicho, Tabora ilikusanya pointi 10 katika mechi nne ikiichapa Yanga mabao 3-1, Mashujaa bao 1-0, KMC 2-0 na kutoka sare ya mabao 2-2 na Singida Black Stars.
Tuzo ya meneja bora wa uwanja imekwenda kwa meneja wa Uwanja wa Lake Tanganyika, Shaaban Rajab kwa kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo na usimamizi wa miundombinu ya uwanjani.
Kwa upande wa Ligi ya Championship, tuzo ya mchezo bora imekwenda kwa Anuar Jabir wakati ile ya kocha bota imekwenda kwa Awadh Juma ambaye kama ilivyo kwa Jabir wote wanatoka Mtibwa Sugar.
Katika kinyang’anyiro hicho Jabir alikuwa akichuana na Naku Kazimoto wa Mbuni na Abdul Aziz Shahame wa TMA wakati Awadh alikuwa akichuana na makocha Salum Mayanga wa Mbeya City na Emmanuel Masawe wa Mbeya Kwanza.
Kimataifa Taoussi ang’ara Novemba
Taoussi ang’ara Novemba
Read also