Na mwandishi wetu
Baada ya kukosekana katika mechi mbili za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025, hatimaye nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amerejeshwa katika kikosi cha timu hiyo licha ya kuwapo habari kwamba anataka kustaafu kuichezea timu hiyo.
Katika orodha ya wachezaji 23 waliotangazwa na kocha wa timu hiyo Hemed Suleiman ‘Morocco’, jina la Simon Msuva kwa mara nyingine halimo kama ilivyo kwa beki Novatus Miroshi ambaye inadaiwa kuwa ni majeruhi.
Stars ambayo tayari imeshacheza mechi mbili za kufuzu Afcon dhidi ya Ethiopia na kutoka sare ya bila kufungana na mechi ya pili dhidi ya Guinea iliyosha kwa Stars kutoka na ushindi wa mabao 2-1.
Kikosi kilichotangazwa leo Jumanne kitakuwa na mechi mbili dhidi ya DR Congo, ambapo timu hiyo itaanzia ugenini Oktoba 10 kabla ya kurudiana Oktoba 15 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Orodha wa wachezaji wa Stars na timu wanazotoka katika mabano ni kama ifuatavyo: Ally Salim (Simba), Zubeir Foba (Azam FC) na Yona Amos (Pamba) ambao ni makipa.
Mabeki: Mohamed Hussein (Simba), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Paschal Msindo (Azam FC) Ibrahim Bacca (Yanga), Bakari Nondo (Yanga), Dickson Job (Yanga), Abdulrazak Hamza (Simba) na Haji Mnoga (Salford FC).
Vingo: Adolf Mtasingwa (Azam FC), Habib Khalid (Singida Black), Himid Mao (Talaal El Geish), Mudathir Yahya (Yanga), Feisal Salum (Azam FC), Suleiman Mwalim (Fountain Gate) na Cyprian Kachwele (Vancouver Whitecaps).
Washambuliaji: Clement Mzize (Yanga), Samatta (Paok FC), Kibu Dennis (Simba), Nassor Saadun (Azam FC) na Abdullah Said (KMC).
Kimataifa Morocco amuita Samatta Stars
Morocco amuita Samatta Stars
Read also
