London, England
Chama cha Soka England au FA kimemkabidhi rasmi beki wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Ashley Cole majukumu ya kocha msaidizi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya wanaume ya England.
Cole ambaye amekuwa akimsaidia kocha wa muda wa timu hiyo, Lee Carsley, mbali na Arsenal na Chelsea lakini pia amewahi kuwa mchezaji tegemeo wa timu ya England akiichezea mara 107.
Tangu mwaka 2021, Cole amekuwa akimsaidia Carsley katika timu ya vijana chini ya miaka 21 ya England ambayo waliiwezesha kubeba taji la Ulaya la vijana U-21 katika mashindano yaliyofanyika Georgia.
Mafanikio hayo bila shaka ndiyo yaliyoishawishi FA kumuamini kuwa mtu sahihi wa kusaidiana na Carsley katika timu ya England ambayo kabla ya hapo ilikuwa ikinolewa na Gareth Southgate.
Kwa mantiki hiyo beki huyo wa zamani wa kushoto sasa atakuwa na makumu mawili kwani mbali na England pia ataendelea na majukumu yake ya ukocha kwenye kikosi cha Birmingham City.
Cole akiwa mchezaji alijipatia umaarufu kwenye kikosi cha England tangu aanze kuichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2001 amekuwa na namba ya kudumu hadi mwaka 2014.
Akiwa na timu hiyo ameshiriki mashindano matano makubwa lakini akiwa na klabu ana rekodi ya kubeba mataji ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012 akiwa na Chelsea.
Kimataifa Ashley Cole rasmi England
Ashley Cole rasmi England
Read also
