Na mwandishi wetu
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Walace Karia amempongeza Mwenyekiti wa Chama cha Soka Arusha (ARFA). Zakayo Mjema (pichani) kwa kuchaguliwa tena kukiongoza chama hicho.
Taarifa ya TFF iliyopatikana leo Jumamosi na kusainiwa na ofisa habari wa shirikisho hilo, Clifford Ndimbo ilimnukuu kiongozi huyo wa TFF akisema kuwa ushindi wa Mjema unaonesha imani ya wajumbe kwake.
Karia alimtaka Mjema ambaye ameshinda katika uchaguzi uliofanyika leo Jumamosi wilayani Longido, kuendelea kusimamia vizuri maendeleo ya mpira wa miguu katika mkoa wa Arusha.
Viongozi wengine waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni James Rugangira aliyeshinda nafasi ya makamu mwenyekiti na Joseph Obedi ambaye ameshinda nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu wa TFF.
Walioshinda nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji ni Athanas Sarwat, Siza Masaka, Hawa Msangi na Engineer Owden ambao wote kwa pamoja wataiongoza ARFA kwa kipindi cha miaka minne ijayo.
Soka Karia ampongeza bosi ARFA
Karia ampongeza bosi ARFA
Read also
