Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa TP Mazembe, Jean Othos Baleke ambaye amewahi kuichezea Simba, ameelezwa kutua Yanga kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja.
Baleke ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Al Ittihad ya Libya, amethibitisha leo Ijumaa kujiunga na Yanga baada ya kuweka picha ya usajili wake wa kutua Yanga katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.
Mshambuliaji huyo, 23 aliyekipiga Simba msimu wa 2022-23 aliweka picha hiyo aliyoitoa kwenye mtandao wa habari wa Africa Transfer Market akiwa amevaa jezi ya Yanga ikionekana kila kitu kimekamilika.
Imeelezwa zaidi kuwa ingawa bado Yanga haijaweka wazi usajili wake lakini tayari Baleke ametua Avic Town, Kigamboni walikoweka kambi Yanga kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
Soka Baleke asaini Yanga kwa mkopo
Baleke asaini Yanga kwa mkopo
Read also
