Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imeendelea kutangaza vifaa vyake vipya kwa siku ya tatu mfululizo na sasa ni zamu ya utambulisho wa Abdulrazack Mohamed Hamza.
Hamza ambaye ni beki wa kati ametua Simba akitokea Supersport FC ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka miwili.
Simba imemtambulisha Hamza kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na kuwa beki wa pili kusajiliwa baada ya mzawa Lameck Lawi aliyetokea Coastal Union.
Hamza ambaye makabrasha yake yanaeleza kuwa na umri wa miaka 21, amewahi kucheza katika klabu za Tanzania; Mbeya City, KMC na Namungo FC, hivyo ana uzoefu wa kutosha na soka la Tanzania.
Mpaka sasa Wekundu hao wametangaza wachezaji watano kuelekea msimu ujao ambapo wengine ni kiungo mshambuliaji wa Ivory Coast, Jean Ahoua, winga wa kulia, Joashua Mutale raia wa Zambia na straika wa Uganda, Steven Mukwala.
Soka Simba yatambulisha beki wa kati
Simba yatambulisha beki wa kati
Read also