Na mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro, amekagua hali ya Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza uliopo kwenye mpango wa kufanyiwa ukarabati mkubwa kwa ajili ya michuano ya Afcon 2027.
Ndumbaro amefanya ukaguzi huo Jumanne hii akiwa ameambatana na Mbunge wa llemela, Angelina Mabula ambapo amekagua eneo la kuchezea, vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji, sehemu za maliwato na eneo la watu mashuhuri.
Ndumbaro amesema mpango wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ni kufanya ukarabati mkubwa wa uwanja huo ambao utatumika kama uwanja wa mazoezi wakati wa Afcon 2027.
Fainali za Afcon 2027 ambazo hushirikisha nchi za mataifa ya Afrika kwa mwaka 2027 zitafanyika katika nchi majirani Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya na Uganda .
Kwa Tazania viwanja vingine vitakavyokarabatiwa ni Jamhuri Morogoro, Uwanja wa Majimaji-Songea, Mkwakwani-Tanga na Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Soka Ndumbaro akagua CCM Kirumba
Ndumbaro akagua CCM Kirumba
Read also
