Na mwandishi wetu
Klabu ya KMC imethibitisha kwa kumtangaza Oscar Paul Mwaigaga (pichani) kama mchezaji wao mpya ambaye wamemnasa kutoka klabu ya Kakamega Home Boys ya Kenya.
Oscar raia wa Tanzania anayemudu nafasi ya kiungo wa kati, alijiunga na Kakamega msimu uliopita akitokea Tanzania Prisons aliyoachana nayo baada ya kumaliza mkataba.
KMC ambayo imemtambulisha Mwaigaga Jumatano hii kupitia majukwaa yake mitandaoni, imeelezwa kumjumuisha nyota huyo kutokana na kiwango alichokionesha Kakamega.
Mei, mwaka huu Mwaigaga alikuwa ni sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyoenda Saudi Arabia kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Sudan.
Klabu hiyo ya Kinondoni pia imeripotiwa kuwa kwenye vita kali ya kuwania saini ya kipa wa Vipers ya Uganda, Fabien Mutombola kipa wa Burundi ambaye pia anawindwa na KCCA ya Uganda na AFC Leopards ya nchini Kenya.
Soka Mwaigaga sasa mali ya KMC
Mwaigaga sasa mali ya KMC
Read also