Na mwandishi wetu
Kocha mpya wa Singida Black Stars, Patrick Aussems amesema malengo makubwa aliyonayo ni kuiongoza timu hiyo kumaliza katika tatu au nne bora kwenye Ligi Kuu NBC msimu wa 2024-25.
Amesema anahitaji kufanya vizuri na kuwepo kwenye hizo nafasi lakini pia kuleta ushindani mkubwa kwa klabu kongwe nchini, Simba na Yanga katika ligi hiyo.
“Nafurahia kuwepo Tanzania kwa mara nyingine, baada ya kuondoka, nilikuwa Afrika Kusini na msimu uliopita nilikuwa Kenya.
“Niseme nilikuwa na ofa nyingi lakini nimeridhishwa na mipango ya Singida Black Stars na kusaini mkataba wa kuinoa timu hii ambayo hata mimi nitapambana kuifikisha kwenye malengo makubwa,” alisema Aussems kocha wa zamani wa Simba.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Singida Black Stars, Jonathan Kasano alisema kwamba timu hiyo imeamua kubadili ratiba ya kambi ambayo awali walipanga kwenda Arusha.
“Tumebadili ratiba yetu ambayo tulipanga kuweka kambi Arusha lakini kwa sababu ya michuano ya Kagame, tunalazimika kubaki Dar es Salaam kufanya maandalizi ya msimu ujao,” alisema.
Soka Aussems aitaka top four ligi kuu
Aussems aitaka top four ligi kuu
Read also
