Los Angeles, Marekani
Brazil imeichapa Paraguay mabao 4-1 katika fainali za Copa America zinazoendelea nchini Marekani katika mechi ya Kundi D ambayo Vinicius Junior ameibuka shujaa kwa kufunga mabao mawili peke yake.
Vinicius Jr ambaye pia ni mshambuliaji wa Real Madrid alifunga bao la kwanza dakika ya 35 kabla Savinho hajaongeza la pili dakika ya 43 na Vinicius kuongeza la tatu katika dakika tano za nyongeza kabla ya mapumziko.
Paraguay wakiwa nyuma kwa mabao matatu walikianza kwa kasi kipindi cha pili na kupata bao lao pekee dakika ya 48 lililofungwa na Omar Alderete lakini walikatishwa tamaa dakika ya 65 baada ya Brazil kufunga bao la nne kwa penalti mfungaji akiwa ni Lucas Paqueta.
Brazil ingeweza kutoka uwanjani na mabao matano lakini Paqueta, kiungo wa West Ham alishindwa kuujaza wavuni mkwaju wa penalti ya awali ambayo ilitolewa dakika ya 30 baada ya beki wa Paraguay kuunawa mpira uliopigwa na Paqueta.
Kwa Vinicius ushindi huo mnono wa jana linakuwa jambo kubwa baada ya kuwataka wachezaji wenzake waboreshe kiwango akionekana kutofurahishwa na matokeo ya sare katika mechi yao iliyopita dhidi ya Costa Rica.
Vinicius kwa mabao hayo anakuwa amefikisha mabao matano akiwa na timu ya Brazil katika mechi 32 na sasa ni kama amefungua ukurasa mpya baada ya kushindwa kuonesha makali yake ya Real Madrid akiwa na timu yake ya taifa.
Katika mechi nyingine ya Copa America ambayo pia ni ya Kundi D iliyochezwa jana Ijumaa, Colombi iliichapa Costa Rica mabao 3-0
Winga wa Liverpool, Luis Diaz ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifungia timu hiyo bao kwa mkwaju wa penalti wakati bao la pili la timu hiyo lilifungwa na beki wa Tottenham, Davinson Sanchez kwa kichwa na la tatu lilifungwa na Jhon Cordoba.
Mechi za Copa America Kundi A kesho Jumapili…
Argentina vs Peru
Canada vs Chile
Kimataifa Vinicius Jr aipendezesha Brazil
Vinicius Jr aipendezesha Brazil
Read also
