Na mwandishi wetu
Imebainishwa kuwa kipa wa kimataifa wa Sudan, Mohamed Mustapha amekamilisha uhamisho wake wa moja kwa moja kutoka Al Marreikh na kutua Azam FC.
Mustapha alijiunga na Azam kwa mkopo wa miezi sita katika dirisha dogo la usajili Desemba, mwaka jana na kuonesha kiwango cha kuridhisha jambo ambalo limewafanya Azam kumuajiri jumla jumla.
Azam imeendelea kuimarisha safu yake ya makipa hasa baada ya makipa wao, Mcomoro, Ali Ahamada, 32 na Mghana, Iddrisu Abdulai, 26 kupata majeraha ya muda mrefu.
Pia, timu hiyo imeendelea kujiweka sawa kutokana na ushiriki wao wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao huku lengo lao likiwa ni kufanya vizuri na kufika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo.
Baada ya kukamilika kwa dili hilo, muda wowote kuanzia leo Jumanne, Azam itathibitisha usajili huo kwani tayari Mustapha ameshawaaga Al Marreikh kupitia andiko lake kwenye mitandao.
Katika andiko hilo lililoonekana leo Jumanne kwenye ukurasa wake wa Instagram, akieleza jinsi gani ataikumbuka klabu hiyo kokote aendako.
Soka Kipa Mustapha rasmi mali ya Azam
Kipa Mustapha rasmi mali ya Azam
Read also
