Na mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa klabu ya Kagera Sugar imeingia kwenye mchakato wa kuiwania saini ya kocha Melis Medo kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa 2024-25.
Taarifa zinafafanua zaidi kuwa Medo raia wa Marekani mwenye asili ya Misri amepokea ofa nyingine kutoka timu za Ligi Kuu NBC na yupo Dar es Salaam kwa sasa kwa mapumziko na kusikiliza ofa alizonazo.
Miezi sita iliyopita, Medo aliachana na Dodoma Jiji akieleza kwenda Dubai kushughulikia matatizo ya kifamilia akiiacha timu hiyo katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Medo aliyewahi kuinoa Coastal Union ya Tanga anatarajia kurithi mikoba ya Fred Felix Minziro aliyepo Tokyo, Japan kwa mapumziko ya mwisho wa msimu wa ligi baada ya kuiongoza Kagera Sugar kumaliza katika nafasi ya 10.
Taarifa hizo hata hivyo hazijaweka wazi ni lini hasa mpango huo utakamilika na kama kocha huyo ameshakubali kibarua hicho.
Soka Medo asubiriwa Kagera Sugar
Medo asubiriwa Kagera Sugar
Read also
