Manchester, England
Utata kuhusu hatma ya kocha Erik Ten Hag wa Man United umekwisha na habari mpya ni kwamba baada ya kufanya tathmini kwa mapana vigogo wa bodi ya klabu hiyo wameamua kocha huyo asiondoke.
Vigogo hao ambao wamekuwa katika zoezi la kumfanyia tathmini Ten Hag na mwenendo wa timu kwa msimu uliopita wa 2023-24, wameama waanze mazungumzo ya kumuongezea mkataba kocha huyo.
Tathmini ya kocha huyo ilianza mara baada ya mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Man City iliyopigwa Mei 25 na Man United kuibuka na ushindi na tayari zilikuwapo habari kwamba kocha huyo angetimuliwa mara tu baada ya mechi hiyo.
Mambo hata hivyo yalibadilika na habari zaidi kudai kwamba ushindi wa mabao 2-1 ambao Man United iliupata katika mechi hiyo na hatimaye kubeba taji huenda ndio uliobadili upepo.
Inadaiwa baada ya tathmini ya kina na mazungumzo yaliyomshirikisha Ten Hag hatimaye muafaka umefikiwa wa kocha huyo Mholanzi mwenye umri wa miaka 54 kuendelea na kibarua chake katika timu hiyo.
Ten Hag bila shaka ataupokea vizuri uamuzi huo hasa baada ya kuwa njia panda kwa muda mrefu akiwa hajui hatma yake kama ataendelea na kibarua chake au angetimuliwa.
Makocha kadhaa tayari walianza kutajwa kuchukua nafasi yake wakiwamo Roberto de Zerbi, Graham Potter, Thomas Frank pamoja na kocha wa sasa wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate.
Ten Hag, alianza kuinoa Man United majira ya kiangazi mwaka 2022 akitokea Ajax, katika msimu wake wa kwanza aliiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England (EPL) pamoja na fainali ya Kombe la FA.
Februari 23, Ten Hag alishinda taji lake la kwanza Man United ambalo ni EFL na msimu huu ingawa amebeba taji la FA lakini mambo hayakuwa mazuri kwenye EPL
Kimataifa Ten Hag haondoki Man United
Ten Hag haondoki Man United
Read also
