Munich, Ujerumani
Kocha wa zamani wa Bayern Munich na Chelsea, Thomas Tuchel ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na Man United amejiweka kando na kazi hiyo kwa alichodai kuwamba kwa sasa anataka kupumzika.
Tuchel, 50, ni kati ya makocha ambao katika siku za karibuni wamekuwa wakipewa nafasi kubwa ya kumrithi Erik Ten Hag ambaye kwa muda mrefu sasa hatma yake Man United ipo njia panda.
Kwa sasa vigogo wa Man United wanafanya tathmini ya mwenendo wa timu yao kwa msimu mzima wa 2023-24 na bado hawajatoa hitimisho la nini kitafanyika kuelekea msimu ujao na hata Ten Hag hajawa na uhakika kama ataendelea kuinoa timu hiyo au la.
Wakati hayo yakiendelea zipo habari kwamba Tuchel aliwahi kukutana na mmiliki mwenza wa Man United Sir Jim Ratcliffe nchini Ufaransa ingawa undani wa mazungumzo ya wawili hao haukuwahi kuwekwa wazi.
Kwa upande wake, Tuchel ambaye pia amewahi kuzinoa klabu za PSG na Borussia Dortmund hata hivyo amedai kwamba kwa sasa anataka kupumzika baada ya kuachana na Bayern mwishoni mwa msimu.
Makocha wengine ambao wamekuwa wakitajwa kuchukua nafasi ya Ten Hag Man United ni pamoja na Graham Potter, Thomas Frank pamoja na kocha wa England, Gareth Southgate.
Kimataifa Tuchel akataa kumrithi Ten Hag
Tuchel akataa kumrithi Ten Hag
Read also
