Na mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa Klabu ya APR ya Rwanda iko kwenye hatua nzuri za kuinasa saini ya nyota wa Yanga SC, Mahaltse Makudubela ‘Skudu’ raia wa Afrika kusini kuelekea msimu ujao.
APR ambao watashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwa mabingwa wa Rwanda, wameonesha kuvutiwa na huduma ya Skudu aliyetua Yanga msimu wa 2023-24 wakiamini atakua sehemu ya msaada kwenye michuano hiyo.
Licha ya mitandao mbalimbali nchini Rwanda kufafanua kuhusu dili hilo lakini pia klabu iliyopanda daraja Afrika Kusini, Magesi FC inatajwa kumhitaji Skudu ambaye mkataba wake na Yanga unafikia ukingoni mwisho wa msimu huu.
Duru mbalimbali zinaeleza kuwa maisha ya Skudu Yanga yamefika mwisho na yumo kwenye orodha ya watakaoachwa katika kikosi hicho kwani amekuwa hapati nafasi ya mara kwa mara chini ya kocha Muargentina, Miguel Gamondi.
Skudu aliyewahi kukipiga Orlando Pirates, Chippa United, Platinum Stars, alisajiliwa Yanga akitokea Marumo Gallants ya Afrika Kusini na kukabidhiwa urithi wa jezi namba sita iliyokuwa ikivaliwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyetimkia Azam FC.
Soka Skudu aelekea APR ya Rwanda
Skudu aelekea APR ya Rwanda
Read also