Istanbul, Uturuki
Kocha wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Jose Mourinho anatarajia kutangazwa rasmi kuwa kocha mkuu mpya wa klabu ya Fenerbahce inayoshiriki Ligi Kuu Uturuki.
Mourinho, 61, atakabidhiwa timu hiyo akichukua nafasi iliyoachwa na Ismail Kartal ambaye juzi Ijumaa aliachana na timu hiyo baada ya kumalizi ligi ikiwa nafasi ya pili nyuma ya mahasimu wao wakuu, Galatasaray.
Klabu hiyo ilionesha picha ya Mourinho kupitia video ambapo kocha huyo alionekana kama akiwasalimia mashabiki na kuwaambia tuonane kesho na kuwataka wajiandae kuianza safari yao pamoja.
Mourinho, ambaye pia amewahi kuzinoa timu za Inter Milan, Man United, Tottenham na FC Porto, amekuwa bila ya kazi tangu atimuliwe na klabu ya Roma ya Italia Januari mwaka huu baada ya kuiongoza kwa nusu ya msimu.
Awali Fenerbahce kupitia mitandao ya kijamii walitoa taarifa ya mazungumzo yao na Mourinho kuhusu kujiandaa kumpa majukumu ya kuinoa timu hiyo kocha huyo Mreno.
Mourinho amewahi kubeba mataji kadhaa yakiwamo ya Ligi Kuu England, Serie A lakini ni kocha pekee mwenye rekodi ya kubeba mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa Ligi na Europa Conference Ligi.
Kimataifa Mourinho asubiriwa Fenerbahce
Mourinho asubiriwa Fenerbahce
Read also