Na mwandishi wetu
Mashabiki visiwani Zanzibar watapata fursa ya kuwaona mastaa wa timu za Yanga na Azam FC kwa kiingilio cha Sh 5,000 kwa viti vya mzunguko vya Uwanja wa New Amaan Complex kunakopigwa fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB.
Kwa mujibu wa tangazo la viingilio vya pambano hilo vilivyowekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya mdhamini wa michuano hiyo, limeonesha kuwa jukwaa la V.I.P ni Sh 30,000.
Viingilio vingine vya pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu linalotarajia kuanza saa 2.15 usiku wa Jumapili, eneo la Wings ni Sh 20,000 wakati Jukwaa la Urusi ni Sh15,000 na lile la Orbit kila shabiki atalipa Sh 10,000.
Ikumbukwe, hilo ni pambano la kwanza la Kombe la Shirikisho Bara kupigwa visiwani Zanzibar na ni la tisa tangu kurejeshwa kwa michuano hiyo rasmi mwaka 2015.
Awali mechi hiyo ilikuwa ipigwe mkoani Manyara lakini baadaye ulifikiwa uamuzi wa kuiondoa kutokana na mazingira kutokuwa mazuri na ndipo uamuzi ulipofikiwa mechi hiyo ichezwe Uwanja wa Amaan ambao umeboreshwa na kuwa katika viwango vya kimataifa.
Soka Buku 5 inatosha kuwaona Yanga, Azam
Buku 5 inatosha kuwaona Yanga, Azam
Read also
