Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki ameeleza kuwa ‘hat-trick’ (mabao matatu) aliyofunga dhidi ya Azam FC ni bora zaidi kuliko aliyowafunga Prisons kwenye mechi ya mwisho ya kufunga pazia la Ligi Kuu NBC.
Mfungaji huyo bora wa ligi kuu msimu huu aliyepachika mabao 21 ameeleza kuwa hat trick ya Azam ilikuwa bora sababu alihitimisha hat-trick hiyo kwa bao la ushindi katika mechi iliyoisha kwa Yanga kutakata kwa mabao 3-2.
“Kwangu bora zaidi ilikuwa dhidi ya Azam sababu tulitangulia kufunga wakachomoa bao, wakaongeza kisha nikafunga tena na kisha nikafunga tena na kupata ushindi, kwangu ushindi ni muhimu zaidi.
“Maana ile ya Prisons ilikuwa ushindi 4-1 na mpaka nafunga bao la mwisho tulikuwa na uhakika wa ushindi, ni tofauti na ile ya Azam maana baada ya wao kufunga bao la pili ilikuwa bado hatuna uhakika lakini nilipofunga la tatu iliibuka furaha kubwa ya uhakika wa pointi tatu,” alifafanua Aziz Ki.
Aziz Ki ambaye ni raia wa Burkina Faso pia amesema hata bao lake bora msimu huu ni bao la tatu alilowafunga Azam kwani sababu kubwa ilikuwa ni namna mashabiki na wadau wao walivyofurahi baada ya mechi ngumu dhidi yao muda wote.
Soka Aziz Ki aikumbuka hat trick ya Azam
Aziz Ki aikumbuka hat trick ya Azam
Read also
