Na mwandishi wetu
Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuihama timu hiyo mpaka atakapohakikisha anatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa Jangwani.
Mchezaji huyo raia wa Burkina Faso ameieleza GreenSports kuwa licha ya taarifa za kuhitajika na timu nyingine lakini ifahamike kuwa hawezi kuhama Yanga mpaka atimize ndoto alizonazo juu ya timu hiyo.
“Mpaka sasa ni mchezaji wa Yanga, najua kuna timu zinanisubiri, wananihitaji lakini muda wote nawapa nafasi Yanga kwanza na nilikuja hapa kwa sababu tunahitaji kuwa juu Afrika, sasa bado tupo kwenye hiyo ‘project’, kwa hiyo mpaka tutakapoikamilisha.
“Ni mpaka tutakapocheza fainali ya Ligi ya Mabingwa hapa Kwa Mkapa (Uwanja wa Benjamin) kisha nitamfuata Rais (Hersi Said) kuulizia baraka zake za kuondoka. Nachopaswa ni kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa na kushinda ubingwa na Yanga, hii ndio ndoto yangu na ndio misheni yangu, nitashinda hili kombe kabla ya kuondoka naamini hilo,” alihitimisha Aziz Ki.
Nyota huyo aliyejiunga na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast ameonesha kiwango kikubwa mpaka sasa akiwa anaongoza kwenye orodha ya mabao Ligi Kuu NBC akifunga mara 18, akifungana kileleni na kiungo wa Azam FC, Feisal Salum.
Aziz Ki ambaye pia anashika namba mbili kwenye orodha ya waliotoa pasi za mabao akiwa nazo nane baada ya Kipre Junior (Azam) mwenye tisa.
Katika siku za hivi karibuni, Aziz Ki amekuwa akitajwa kuwindwa na vigogo wa Afrika wakiwemo Mamelodi Sundowns, Kaizer Chiefs, Al Ahly na Pyramids ikielezwa wako tayari kutoa kitita kunasa saini ya mchezaji huyo.
Soka Aziz Ki haondoki Yanga hadi abebe taji Ligi ya Mabingwa
Aziz Ki haondoki Yanga hadi abebe taji Ligi ya Mabingwa
Read also