Madrid, Hispania
Klabu ya Real Madrid inadaiwa ipo katika hatua za mwisho kumsainisha mkataba mpya kiungo wake mkongwe Luka Modric pamoja na mastaa wengine.
Mastaa wengine wanaotajwa kuwa katika mpango huo ni beki Lucas Vázquez na kipa Andriy Lunin ingawa inadaiwa pia kuna mjadala kuhusu majaliwa ya nahodha wa timu hiyo, Nacho Fernandez.
Katika mpango huo wakati Modric ambaye kwa sasa ana miaka 38 akifikiriwa kupewa mkataba wa mwaka mmoja zaidi kama ilivyo kwa Vázquez, 32, Lunin, 25 yeye anatarajia kusaini mkataba ambao utafikia ukomo mwaka 2029.
Kuhusu Modric, mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or ilitarajiwa angeachana na timu hiyo mara baada ya msimu huu lakini kutokana na umuhimu wake ndani na nje ya uwanja, klabu hiyo na kocha Carlo Ancelotti wameona ni bora waendelee kuwa naye.
Uzoefu mkubwa wa Modric na umuhimu wake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kukubali kwake majukumu ikiwamo kuwa mchezaji wa akiba mwenye mchango muhimu ni kati ya mambo yaliyoifanya klabu ibadili msimamo na kuanza mchakato wa kumpa mkataba mpya.
Pia inadaiwa kuwa Modric mwenyewe anapenda zaidi kuendelea kuichezea Real Madrid na wala hajashawishika na ofa za kwenda kwingineko ikiwamo Saudi Arabia.
Kimataifa Modric kuongezewa mkataba Real Madrid
Modric kuongezewa mkataba Real Madrid
Read also
