Na mwandishi wetu
Serikali ya Tanzania imesema ujenzi wa viwanja vipya vya michezo kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2027), unatarajiwa kukamilika mwakani ili kupisha ukaguzi wa kikanuni wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
Hayo yameelezwa kutokana na uandaaji wa michuano hiyo kupitia nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda zilizoomba kushiriki kwa kuandaa kwa pamoja michuano hiyo mikubwa Afrika ikiwa pia ni mara ya kwanza nchi hizo zinafanya hivyo.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwijuma amefafanua kuhusiana hilo leo Jumanne wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chakechake, Ramadhan Suleiman Ramadhan.
Mbunge huyo alihoji ni lini viwanja vipya ambavyo Serikali inatarajia kujenga kwa ajili ya matayarisho ya Afcon vitakamilika.
Akijibu swali hilo, Mwijuma alisema kwa mujibu wa ratiba na mahitaji, viwanja hivyo vinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka ujao na kwamba wanafanya hivyo ikiwa ni tayari kwa ajili ya ukaguzi wa kikanuni ambao utafanyika mwakani.
Mpaka sasa Tanzania inatarajia kutumia viwanja vitatu katika michuano hiyo ambavyo ni Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa New Amaan Complex wa Zanzibar na uwanja mpya wa kisasa unaojengwa jijini Arusha.
Kimataifa Viwanja vya Afcon kukamilika mwakani
Viwanja vya Afcon kukamilika mwakani
Read also
