Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema anatambua wapinzani wao katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB, Yanga wana wachezaji hatari lakini hata wao pia wana wachezaji wenye ubora mkubwa wa kuamua matokeo.
Maxime ameyasema hayo leo Jumamosi kuelekea mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha ambapo amesisitiza kuwa anafahamu ushindi wao utatokana na umoja wakishirikiana kudhibiti, kukaba na kushambulia kwa pamoja kama timu.
“Kikubwa kwanza kwenye timu kuwa kitimu kimpira na sio walinzi peke yao ndio wafanye kazi ya kuzuia, yaani mnazuia kama timu na hiyo inakuwa pale mpira mnaponyang’anywa ndipo mara moja mnapoanza kufanya ulinzi.
“Japo tunafahamu Yanga ina wachezaji wazuri kama alivyosema mwalimu wao (Miguel Gamondi), wachezaji hatari ambao nafasi moja mbili wanakumaliza.
“Sasa Ihefu pia ina wachezaji bora na sasa hivi tupo kwenye muunganiko mzuri toafuti na mwanzo, sasa hivi timu imeshasimama kwa hiyo na sisi pia tunao watu ambao wanaweza kumaliza mechi.
“Kikubwa Yanga wanakimbia sana, sasa ili kwenda nao sawa lazima na wewe ubora wa kazi yako uwe mkubwa sana, kitu ambacho naamini tutakwenda kukifanya hiyo kesho,” alisema Maxime.
Soka Maxime ajivunia ubora Ihefu akiivaa Yanga
Maxime ajivunia ubora Ihefu akiivaa Yanga
Read also
