Manchester, England
Klabu ya Manchester United inadaiwa haina mpango wa kumtimua kocha wake, Erik ten Hag kwa wakati huu badala yake jambo hilo lifanyika mara tu baada ya mechi ya fainali ya Kombe la FA itakayopigwa Mei 25.
Man United itaumana na Man City katika mechi ya fainali ya Kombe la FA, mechi ambayo huenda ikaifanya timu hiyo ibebe taji lake la kwanza msimu huu kama itafanikiwa kuibuka na ushindi.
Majaliwa ya Ten Hag katika kikosi cha Man United yamekuwa njia panda kwa sababu ya matokeo mabaya na zimekuwapo habari kwamba angetimuliwa wakati wowote lakini kwa sasa kilicho wazi ni kwamba hatua hiyo itafikiwa baada ya mechi na Man City.
Wakati hali ikiwa hivyo kwa Ten Hag chanzo kimoja cha habari kimedai kuwa kocha wa Bayern Munich ambaye ataachana na timu hiyo baada ya msimu huu, Thomas Tuchel inadaiwa anaitamani fursa ya kuinoa Man United.
Wengine ambao vyombo kadhaa vya habari vimekuwa vikiwataja kuwa wanaweza kupewa nafasi ya kumrithi Ten Hag ni kocha wa Sporting Lisbon, Ruben Amorin na Graham Potter ambaye aliwahi kuinoa Chelsea.
Kocha mwingine anayetajwa ni Jose Mourinho ambaye kama atapewa nafasi hiyo atakuwa anarudi kwa mara ya pili, hivi karibuni alinukuliwa akisema kwamba wakati akiinoa Man United hakuwa akipata ushirikiano wa kutosha kwa mabosi wake.
Mourinho ambaye ametimuliwa na klabu ya Roma ya Italia, alisema anaamini kukosa ushirikiano kulichangia kumkwaza katika kazi yake.
Kimataifa Ten Hag kutimuliwa Mei 25
Ten Hag kutimuliwa Mei 25
Read also