Na mwandishi wetu
Simba imefanikiwa kunyakua pointi tatu baada ya kuichapa Tabora United mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa Jumatatu hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Ushindi huo umeifanya Simba kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya mahasimu wao Yanga kutoka 15 za awali na sasa inakuwa imezidiwa na Yanga yenye pointi 65 kwa tofauti ya pointi 12.
Simba hata hivyo pamoja na ushindi huo wanaendelea kubaki nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa wametanguliwa na Azam FC yenye pointi 57 ingawa Simba wamecheza mechi 24 dhidi ya 25 za Azam.
Mabao ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na Kanoute katika dakika ya 19 wakati bao la pili na la ushindi lilifungwa na Edwin Balua.
Kwa Tabora Utd, matokeo hayo yanazidi kuwaweka pagumu kwani hadi sasa wameweza kuvuna pointi 23 katika mechi 25 hivyo wana kazi ya kujinasua na janga la kushuka daraja katika ligi hiyo yenye timu 16.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa Jumatatu hii, Azam ilitoka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Mtibwa Sugar mabao ya washindi yakifungwa na Feisal Salum na Girbil Sillah wakati Coastal Union na Prisons zilitoka sare ya 0-0.
Soka Simba yaitandika Tabora Utd 2-0
Simba yaitandika Tabora Utd 2-0
Read also
