Na mwandishi wetu
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imezipongeza timu za Ken Gold ya Mbeya na Pamba ya Mwanza kwa kufanikiwa kupanda daraja kutoka Ligi ya Championship hadi Ligi Kuu NBC msimu ujao wa 2024-25.
Ofisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda amesema timu hizo zinastahili pongezi za dhati kwa sababu zimepanda kushiriki ligi kuu katika msimu ambao ulionekana kuwa na upinzani mkubwa kwa timu zote shiriki.
“Tunapenda kuzipongeza timu za Ken Gold na Pamba kwa kupanda kushiriki Ligi Kuu NBC msimu ujao, zimepanda katika msimu ambao naweza kusema ulikuwa wa moto sana, msimu ambao mpaka siku ya mwisho kulikuwa na timu moja tu ambayo imekata tiketi ya kushiriki ligi kuu.
“Yaani kuna timu nyingine tatu zilikuwa na nafasi ya kukata tiketi hiyo, kwa hiyo utaona namna gani ulikuwa msimu mgumu na kwa niaba ya Bodi ya Ligi tunawapongeza kwa kupanda daraja lakini pia tunazipongeza timu nyingine pia maana hata hizo ambazo hazikupata nafasi ya kupanda zilifanya jitihada kubwa lakini kutokana na ushindani mkubwa ndiyo imeshindikana wao kufanya hivyo,” alisema Boimanda.
Soka TPLB yazipongeza Ken Gold, Pamba
TPLB yazipongeza Ken Gold, Pamba
Read also
