Manchester, England
Kipa wa Man United, Andre Onana amefanya makosa yaliyozaa penalti katika dakika ya 87 na kuifanya timu yake itoke sare ya 1-1 na Burnley katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) jana Jumamosi.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Old Trafford, Man United ilipata bao la kuongoza dakika ya 79 lililofungwa na Antony lakini dakika tatu kabla ya kutimia dakika 90, Burnley walipata bao la penalti iliyopigwa na Zeki Amdouni.
Man United katika mechi hiyo ingawa haikuonesha ubora lakini juhudi za Antony ziliibua matumaini ya kutoka uwanjani na pointi tatu kabla mambo hayajaharibika baada ya Onana kumchezea rafu mchezaji wa Burnley wakati akiokoa hatari iliyoelekezwa langoni mwake.
Rafu hiyo ilionekana baada ya matumizi ya VAR na ndipo Amdouni aliyeingia kipindi cha pili akafunga bao baada ya kumchanganya Onana aliyeruka upande tofauti na mpira ulipokwenda.
Matokeo hayo yanakuwa faraja kubwa kwa Burnley ambayo inapambana kujinasua na janga la kushuka daraja ikiwa imejitenga na janga hilo kwa tofauti ya pointi mbili huku Man United ikijiweka pagumu kusaka tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Burnley inayonolewa na mchezaji wa zamani wa Man City, Vincent Kompany wiki ijayo itakuwa na kibarua dhidi ya Newcastle wakati mechi yake ya mwisho ya msimu itacheza na Nottingham timu nyingine iliyo katika hatari ya kushuka daraja.
Matokeo ya mechi za EPL Jumamosi…
West Ham 2-2 Liverpool
Fulham 1-1 Crystal Palace
Man Utd 1-1 Burnley
Newcastle 5-1 Sheff Utd
Wolves 2-1 Luton
Everton 1-0 Brentford
Aston Villa 2-2 Chelsea
Kimataifa Onana alikoroga Man United
Onana alikoroga Man United
Read also
