Munich, Ujerumani
Bayern Munich ipo mbioni kumuajiri, Ralf Rangnick (pichani) kuwa kocha mpya wa timu hiyo ingawa kuna habari kuwa Rangnick huenda akaifanya kazi hiyo kwa msimu mmoja kabla ya kumpisha Jurgen Klopp katika msimu wa 2025-26
Chanzo kimoja cha habari nchini Ujerumani kimedai kuwa Rangnick atachukua nafasi ya Thomas Tuchel ambaye ataachana na timu hiyo baada ya msimu huu lakini atakuwa kocha wa mpito na kuinoa timu hiyo kwa msimu wa 2024-25 tu.
Bayern awali ilikuwa ikimtaka Xabi Alonso anayeinoa Bayer Leverkusen achukue nafasi ya Tuchel lakini Alonso alikataa kwa alichosema kwamba anadhani bado anahitaji kufanya kazi Leverkusen.
Uamuzi huo uliifanya Bayern kumpigia hesabu Klopp ambaye Januari mwaka huu alitangaza kuwa ataachana na Liverpool baada ya msimu huu ingawa Klopp inadaiwa anataka kupata mapumziko ya walau msimu mmoja kabla ya kurudi tena kwenye kazi ya ukocha.
Kwa mantiki hiyo kumpata Klopp ni baada ya msimu wa 2024-25 na hilo limewafanya Bayern waelekeze nguvu zao kwa Rangnick ambaye ni mzoefu na Ligi Kuu Ujerumani yaani Bundesliga kwani aliwahi kuwa kocha wa RB Leipzig.
Hata hivyo haijaweza kueleweka mara moja iwapo Rangnick ambaye kwa sasa anainoa timu ya taifa ya Austria atakubali mkataba ambao utamuweka kibaruani kwa msimu mmoja kabla ya kumpisha Klopp atakayekuwa kocha wa kudumu.
Hapo hapo kuna ukweli kwamba Rangnick pia anaweza kupewa kibarua Bayern na wakati huo huo akaendelea kibarua chake cha sasa kwenye timu ya Austria na hivyo kufanya kazi zote mbili pamoja.
Kazi ya timu ya taifa haina mapambano ya kila wiki kama ilivyo klabu ambayo inakuwa na mechi moja au mbili kwa wiki na hivyo Rangnick anaweza kuajiriwa kama kocha wa muda ingawa bado suala la kocha huyo kufanya kazi mbili linaweza kuwatesa wakurugenzi wa Bayern.
Kimataifa Rangnick kumsafishia Klopp kiti Bayern?
Rangnick kumsafishia Klopp kiti Bayern?
Related posts
Read also
