Paris, Ufaransa
Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane au Zizou inadaiwa anafuatilia kwa karibu kinachoendelea kwa kocha wa Man United, Erik ten Hag na angependa kuinoa timu hiyo kuliko Bayern Munich.
Zizou ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, amekuwa hana kazi kwa kipindi kirefu tangu kufeli kwa mpango uliodaiwa wa yeye kuinoa timu ya taifa ya Ufaransa.
Chanzo kimoja cha habari nchini Ufaransa kimeeleza kuwa Zizou ambaye amewahi pia kuhusishwa na mpango wa kuinoa Bayern Munich na ingawa klabu hiyo haijawasiliana naye rasmi lakini mwenyewe inadaiwa angependa zaidi kuinoa Man United.
Zizou amejipatia mafanikio makubwa akiwa mchezaji wa Real Madrid kwa kubeba mataji kadhaa likiwamo la Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kugeukia ukocha na kujipatia heshima nyingine kwa kubeba taji hilo hilo hilo na Real Madrid.
Kocha huyo hata hivyo baada ya hapo amekuwa hana kazi licha ya kuhusishwa na klabu kadhaa ikiwamo PSG pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa, mipango ambayo yote ilifeli lakini kwa sasa ameanza kuhusishwa na klabu za Bayern Munich na Man United.
Bayern inasaka kocha wa kumrithi Thomas Tuchel ambaye mkataba wake umesitishwa na huu ni msimu wake wa mwisho na timu hiyo wakati Man United inadaiwa kuwa mbioni kufanya mabadiliko makubwa.
Mabadiliko hayo yanayosimamiwa na mmiliki mwenza mpya wa klabu hiyo bilionea, Sir Jim Ratcliffe yameshaanza kufanywa na huenda yakamkuta Ten Hag hasa kwa kuwa mwenendo wa timu hiyo si mzuri kwa sasa.
Kimataifa Zizou aipigia hesabu Man United
Zizou aipigia hesabu Man United
Read also