Turin, Italia
Mahakama ya Michezo nchini Italia imeitaka klabu ya Juventus kumlipa winga wa zamani wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo Pauni 8.3 milioni za mshahara alizokuwa akidai.
Ronaldo, 39 ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Al Nasr ya Saudi Arabia, alikubali kucheleweshewa mshahara na klabu hiyo wakati wa kipindi cha janga la korona.
Awali Ronaldo ambaye alijiunga na Juventus mwaka 2018 akitokea Real Madrid na kudumu hadi mwaka 2021, alidai kwamba alikuwa akiidai klabu hiyo Pauni 17 milioni.
Mahakama hiyo katika uamuzi wake iliridhia mchezaji huyo aliyeisaidia Juventus kubeba mataji ya Serie A mara tano kulipwa kiasi chote alichokuwa akidai baada ya kukatwa kodi.
Ronaldo, mshindi wa tuzo za Ballon d’Or mara tano, aliachana na Juventus na kurudi katika klabu yake ya zamani ya Manchester United ambayo alidumu nayo kwa miezi 16 kabla ya kutimkia Saudi Arabia alipojiunga na Al Nasr anayoichezea hadi sasa.
Kimataifa Juve yatakiwa kumlipa Ronaldo chake
Juve yatakiwa kumlipa Ronaldo chake
Read also
