Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ amekiri kuwa hali waliyonayo kwenye Ligi Kuu NBC ni ngumu lakini watahakikisha wanaanza kukaa vyema kupitia mechi yao ya Jumatano hii dhidi ya Azam FC.
Baresi amezungumza hayo Jumanne hii jijini Dar es Salaam akifafanua kuwa kikosi chake kipo kwenye morali nzuri ya mchezo tangu walipowasili Dar es Salaam.
Kocha huyo alikiri kuwa timu yake inafahamu kuhusu ubora wa Azam lakini watapambana kupata matokeo na kujiweka kwenye nafasi nzuri.
“Tumepoteza mechi mbili zilizopita na kabla ya hapo tulikuwa tunaenda vizuri na sasa hatuna hali nzuri kwenye ligi hivyo tunapambana na tuko sawa kuhakikisha tunapata matokeo mchezo wa kesho. Tunajua Azam ni timu nzuri wana kikosi kizuri hivyo hautakuwa mchezo rahisi lakini nasi tutacheza kwa ubora wetu tukihitaji matokeo.
Katika mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 2.30 usiku, Mashujaa itaingia dimbani ikiwa na pointi 21, nafasi ya 15 baada ya mechi 22.
Kwa upande wa Azam timu hiyo pia imecheza idadi ya mechi kama za Mashujaa lakini wao wanashikilia nafasi ya pili wakiwa wamekusanya pointi 50.
Soka Baresi akiri ugumu, ajipa matumaini
Baresi akiri ugumu, ajipa matumaini
Read also
