Paris, Ufaransa
Kocha wa PSG, Luis Enrique amesema anaamini timu yake inaweza kupindua meza na kuibuka na ushindi katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona itakayopigwa leo Jumanne.
Katikam mechi ya kwanza iliyopigwa mjini Paris, Barca iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, matokeo ambayo pia yaliifanya PSG ibaki na rekodi ya kucheza mechi 27 za mashindano yote bila kupoteza hata moja.
Enrique alikuwa kocha wa Barça mwaka 2017 na kufanikiwa kupindua meza baada ya kufungwa mabao 4-0 na PSG lakini katika mechi ya pili waliichapa PSG 6-1 na sasa kocha huyo anataka jambo hilo lijirudie akiwa kocha PSG.
“PSG haijawahi kupindua meza baada ya kufungwa katika mechi ya kwanza, lakini Jumanne ndio siku ya kufanya hivyo,” alisema Enrique katika mkutano na waandishi wa habari.
“Baada ya kupoteza mechi muhimu, baada ya mechi hiyo mambo yanakuwa magumu, ni mtego fulani, kunakuwa na ugumu kujiweka sawa kisaikolojia lakini jambo zuri katika soka ni kwamba baada ya hapo unakuwa na mechi nyingine dhidi ya mpinzani yule yule,” alisema Enrique.
Kabla ya mechi ya kwanza baina ya timu hizo, Enrique anakumbukwa kwa kusema kwamba analijua vyema soka la Barca kumzidi kocha wa sasa wa timu hiyo, Xavi Hernandez na msimamo wake utaendelea kuwa hivyo ingawa hiyo haimaanishi kwamba haheshimu kazi ya Xavi.
Kwa upande wake, Xavi yeye alisema kwamba anamuweka Enrique kwa ubora sawa na makocha wa kiwango cha juu kina Pep Guardiola na Luis Aragones na kwake kati ya makocha bora waliowahi kumfundisha.
Xavi ambaye leo ana faida ya kuwa nyumbani, aliwahi kucheza soka na Enrique wakiwa Barça na baadaye katika msimu wa 2014-15, Enrique alikuwa kocha wa Barca, Xavi akiwa mchezaji.
Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya leo Jumanne
Barca v PSG
B Dortmund v Atl Madrid
Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho Jumatano
Bayern Munich v Arsenal
Man City v Real Madrid
Kimataifa Enrique aamini PSG itaizamisha Barca
Enrique aamini PSG itaizamisha Barca
Read also
