Barcelona, Hispania
Beki wa zamani wa klabu za Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves ameonesha jeuri ya fedha baada ya kumrudishia baba mzazi wa Neymar Euro 150,000 ambazo alimpa zimsaidie katika kesi ya kubaka inayomkabili.
Alves anakabiliwa na kesi ya udhalilishaji kijinsia akidaiwa kubaka msichana katika klabu moja ya usiku mjini Barcelona na tayari amekutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha jela miaka minne na nusu.
Chanzo kimoja cha habari nchini Ufaransa kupitia wakili wa mchezaji huyo kilithibitisha Alhamisi hii kuwa Alves ambaye kwa sasa yuko nje kwa dhamana amerudisha kiasi hicho cha fedha tangu wiki iliyopita.
Alves, 40, Februari 22 alihukumiwa katika mahakama moja ya juu ya Calatonia baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka msichana huyo, kosa analodaiwa kulifanya usiku mmoja wa Desemba, 2022 baada ya kumnunulia pombe.
Machi 25 mwaka huu Alves alitolewa kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya ikiwamo kutoa kiasi cha Euro 1 milioni huku akiendelea kusikiliza matokeo ya rufaa aliyokata ingawa alisota gerezani miezi 14 tangu kukamatwa kwa kosa linalomkabili.
Alves na Neymar waliwahi kucheza pamoja Barca na timu ya taifa ya Brazil na kwa muda mfupi katika klabu ya PSG na baada ya kukumbwa na mkasa huo, familia ya Neymar kupitia baba yake mzazi iliahidi kumsaidia.
Wakati Alves akipigania kuachiwa huru, waendesha mashtaka wameshikilia msimamo wa kutaka afungwe miaka tisa jela wakati wakili wa msichana anayedaiwa kubakwa anataka mchezaji huyo afungwe miaka 12 jela.
Alves inadaiwa alimbaka msichana huyo baada ya kumnunulia pombe na kumualika katika chumba cha watu maarufu kwenye klabu hiyo ya usiku na kutumia nguvu kufanya kitendo hicho licha ya msichana huyo kumsihi asifanye hivyo lakini hakumsikiliza.
Kimataifa Alves amrudishia Baba wa Neymar fedha zake
Alves amrudishia Baba wa Neymar fedha zake
Read also
