Na mwandishi wetu
Baada ya dakika 90 za kukata na shoka kumalizika kwa sare ya 0-0 hatimaye Yanga imeziaga fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulala kwa penalti 3-2 mbele ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Katika mechi hiyo ya marudiano iliyochezwa leo Ijumaa mjini Pretoria, Yanga ilihitaji ushindi wowote au sare ya mabao ili kusonga mbele baada ya sare ya 0-0 katika mechi ya kwanza iliyopigwa jijini Dar es Salaam.
Waliokosa penalti za Yanga ni Stephanie Aziz Ki ambaye alikuwa wa kwanza kupiga penalti lakini mkwaju wake aliouelekeza upande wa kushoto wa kipa Ronwen Williams uliokolewa na kipa huyo.
Wachezaji wengine wa Yanga waliokosa penalti ni Dickson Job na Ibrahim Bacca ambaye alipiga penalti ya mwisho ya Yanga iliyohitimisha safari ya timu hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Waliopata penalti kwa upande wa Yanga ni Augustine Okrah aliyepiga shuti kali la kiufundi la mguu wa kushoto pamoja na Joseph Guede.
Kwa upande wa Mamelodi penalti zao zilifungwa na Allende, Libeiro na Maema wakati Sirinyi shuti lake liliokolewa na kipa Djigui Diarra wa Yanga.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kushindwa kuweka rekodi iliyokuwa ikiisaka ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo licha ya matumaini makubwa yaliyokuwapo kabla ya mechi hiyo.
Yanga hata hivyo ilizicheza kwa umakini dakika 90 za awali kwani licha ya Sundowns kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa na kufanya mashambulizi mengi bado ilikuwa vigumu kuipenya safu ya ulinzi ya Yanga.
Katika dakika ya 59, Aziz Ki aliunasa mpira na kumpasia Kennedy Musonda ambaye alimrudishia Aziz Ki na kufumua shuti kali la mguu wa kushoto ambalo liligonga mwamba wa juu na kurudi uwanjani.
Shuti hilo lilizua kizaazaa ambapo kwa macho ya mashabiki walio wengi mpira huo ulionekana kuvuka mstari wa goli lakini baadaye mwamuzi alijirdhisha na kuamuru kuwa halikuwa goli.
Yanga pia ilifanya mashambulizi mengine dakika za 32 lakini shuti la chinichini lililopigwa na Guede kutokana na pasi ya Maxi Nzengeli lilitoka nje ya lango
Baadaye Mzize naye aliunganishiwa pasi nzuri na Aziz Ki lakini alishindwa kuujaza mpira wavuni akiwa karibu na lango la Mamelodi.
Katika mechi hiyo kocha Miguel Gamondi kwa nyakati tofauti aliwatoa Mwamnyeto na kumuingiza Fred Gift, Kennedy Musonda na kumuingiza Clement Mzize na baadaye akawatoa Maxi Nzengeli na Lomalisa na nafasi zao kuingia Okrah na Kibabage.
Kimataifa Mamelodi yaitoa Yanga kwa penalti 3-2
Mamelodi yaitoa Yanga kwa penalti 3-2
Read also
