Na mwandishi wetu
Benki ya CRDB imeingia mkataba wa miaka mitatu na nusu wenye thamani ya Sh bilioni 3.79 kwa ajili ya udhamini wa michuano ya Kombe la FA.
Mkataba huo umesainiwa leo Jumanne katika makao makuu ya benki hiyo, Dar es Salaam chini ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, AbdulMajid Nsekela.
Kutokana na mkataba huo, michuano hiyo inayoshirikisha timu zaidi ya 100 kuanzia ngazi ya wilaya, itaanza kufahamika kwa jina la CRDB Bank Confederation Cup katika hatua ya 16 bora msimu huu wa 2023-24.
Akizungumza katika hafla hiyo, Karia alisema: “Ni tukio la kishitoria la mdhamini mkuu mpya au wa kwanza wa Kombe la shirikisho, nikimaanisha tulikuwa tunaita Azam Sports Federation Cup sababu tulimpa Azam kutokana na urushaji matangazo lakini sasa tumempata mdhamini wa kwanza wa michuano hii na ni CRDB, nawapongeza katika hilo kwa kuiongeza thamani ya soka nchini.”
Soka CRDB yamwaga bilioni 3 Kombe la FA
CRDB yamwaga bilioni 3 Kombe la FA
Read also
