Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi amesema Simba ina uwezo wa kuifunga Al Ahly kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kutokana na timu hizo kukutana mara nyingi.
Okwi aliyewahi kuitumikia Simba kwa vipindi vitatu tofauti kuanzia 2009-13, 2014-15 na 2017-19 alisema pamoja na ukubwa wa Al Ahly lakini haoni kama mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika wanaweza kuondoka na ushindi kutokana na jinsi rekodi zilivyo.
“Al Ahly imekuja Tanzania mara nyingi miaka ya karibuni lakini imeshindwa kuondoka na ushindi hivyo safari hii watakuja kwa nguvu zaidi kwani wanataka kutetea ubingwa wao, lakini Simba ina rekodi nzuri Uwanja wa Mkapa, imezifunga timu nyingi lakini wachezaji wanapaswa kutambua umuhimu wa mchezo ulio mbele yao hivyo wajitume na kufuata maelekezo ya mwalimu,” alisema Okwi.
Alisema wachezaji hawapaswi kuwahofia wapinzani wao bali wanatakiwa kucheza kwa kujituma na kufuata kile ambacho wameelekezwa na makocha wao kama hilo likifanyika anaamini Al Ahly atapoteza mchezo huo.
Aliongeza kuwa kikosi cha Simba kina wachezaji wakubwa na wazoefu wa mashindano makubwa hivyo wanapaswa kutumia kila nafasi watakazopata lakini pia wasifanye makosa kwenye eneo la ulinzi.
Soka Okwi aipa ushindi Simba kwa Ahly
Okwi aipa ushindi Simba kwa Ahly
Read also
