Na mwandishi wetu
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Meshack Mwankemwa amesema kuwa maandalizi ya pambano lake la kuwania ubingwa wa World Boxing Foundation International Middleweight (WBF) dhidi ya Rayton Okwiri wa Kenya, yamekamilika kilichobaki ni kwenda kuimaliza kazi ulingoni.
Pambano hilo la raundi 10 litafanyika ukumbi wa Chartel, Nairobi, Kenya ambapo Mwankemwa ataingia ulingoni akiwa na kumbukumbu ya kushinda pambano lake la mwisho kwa KO kwa kumchapa Said Hamdan, Februari 3, mwaka huu.
Akizungumza Jumatatu hii, Mwankemwa alisema anajua kiu ya mashabiki wake ni kuona anaibuka na ushindi katika pambano lijalo ili kuendeleza ubabe wake Afrika pamoja na kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mchezo wa ngumi.
“Najua mashabiki wangu wanatamani kuona kile kilichotokea katika michezo iliyopita, nawaahidi kuwa pambano hili litakuwa la kuweka heshima na kurudi nyumbani na mkanda,” alisema.
Ngumi Mwankemwa atamba kumchapa Okwiri
Mwankemwa atamba kumchapa Okwiri
Related posts
Read also
