Na mwandishi wetu
Kinara wa mabao kwenye kikosi cha KMC, Wazir Junior amesema siri ya ubora alionao msimu huu ni kutokana na kumsikiliza kwa umakini kocha wake Abdulhamid Moallin.
Mshambuliaji huyo ambaye alifunga ‘hat-trick’ timu yake ilipoibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Tabora United na kufikisha jumla ya mabao 11 msimu huu akiwa na Watoza Ushuru hao wa Manispaa ya Kinondoni.
Waziri Jr ambaye pia ni mshambuliaji wa zamani wa Yanga alisema amekuwa akifuata kikamilifu mbinu anazopewa na kocha wake na anashukuru Mungu mambo yake yanakwenda vizuri msimu huu.
“Namshukuru kocha Moallin mbinu zake ndio zinanifanya nionekane bora leo lakini ni vyema watu wakajua siri ya ubora nilionao msimu huu unatokana na kusikiliza kwa umakini maelekezo ya kocha na ushirikiano mzuri na wachezaji wenzangu,” alisema Wazir.
Alisema pamoja na kufikisha mabao ambayo yamemfanya kupnda juu kwenye orodha ya wafungaji, bado hajafikiria kubeba tuzo ya mfungaji bora kutokana na wapinzani anaoshindana nao Feisal Salum wa Azam FC na Stephane Aziz Ki wa Yanga.
Waziri Jr, maarufu kwa jina la King of CCM Kirumba, tangu ajiunge na KMC mwanzoni mwa msimu huu akitokea Dodoma Jiji amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho.
Mabao ya mshambuliaji huyo yameipandisha timu hiyo kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC ikiwa sasa inapambana kupata nafasi ya kushiriki msimu ujao michuano ya klabu Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Soka Waziri Jr ataja siri ya mabao yake
Waziri Jr ataja siri ya mabao yake
Read also