Na mwandishi wetu
Simba imeipa kipigo cha mabao 3-1, Singida Fountain Gate katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa Jumatatu hii kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Alikuwa ni kiungo mshambuliaji wa Simba, Saido Ntibazonkiza mbaye aliandika mabao mawili, la kwanza katika dakika ya sita na la pili dakika tatu baadaye kwa mkwaju wa penalti.
Zikiwa zimebaki dakika 10 kabla ya timu kwenda mapumziko Simba walifanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na Freddy Koublan na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 3-0.
Singida FG haikukatishwa tamaa na mabao hayo na juhudi za timu hiyo zilizaa matunda dakika sita kabla ya kutimia dakika 90 ilipopata bao pekee la kufutia machozi lililofungwa na Thomas Ulimwengu.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 42 katika mechi 18 ikibaki katika nafasi ya tatu ikiwa imetanguliwa na Azam iliyo nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi 44 wakati Yanga inashika usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 49.
Kwa upande wa Singida FG, timu hiyo inaendelea kusalia katika nafasi ya 11 ikiwa imekusanya ponti 21 katika mechi 20 ilizocheza hadi sasa.
Soka Simba yaipa kipigo Singida FG
Simba yaipa kipigo Singida FG
Read also
