Na mwandishi wetu
Klabu ya Singida Fountain Gate FC leo Jumatano imemtambulisha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kuwa kocha mkuu wa timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu.
Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, John Kadutu alisema wamechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi hicho kilipokuwa chini ya Thabo Senong na msaidizi wake, Nizar Khalfan.
“Tumempa mkataba wa muda mfupi Julio hadi mwisho wa msimu huu ili kuangalia mwenendo wa timu katika mechi 10 zilizobaki kabla ya msimu kumalizika baada ya hapo kama tutafanikiwa kubaki lgi kuu tutampa mkataba mrefu pamoja na kufanya usajili wa nguvu kuimarisha kikosi chetu,” alisema Kadutu.
Kiongozi huyo alisema mbali ya Julio, pia imembakisha Ngawina Ngawina katika nafasi ya kocha msaidizi na pia wamemchukua Ally Mustapha ‘Bartherz’ kuwa kocha wao wa makipa.
Kadutu alisema wana imani kubwa na Julio kutokana na uzoefu wake kwenye Ligi Kuu NBC na kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya waliyokuwa wakiyapata tangu mwanzo wa mwaka huu.
Kiongozi huyo alisema kwamba wanaamini mchezo ujao dhidi ya Namungo FC watapata ushindi wao wa kwanza.
Singida FG ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 21 katika mechi zake 20 ilizoshuka dimbani mpaka sasa.
Soka Julio akabidhiwa mikoba Singida
Julio akabidhiwa mikoba Singida
Read also
